ZIARA YA MRATIBU ZANZIBAR KWA WANACHAMA WA MTANDAO.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - Zanzibar (THRDC Zanzibar) imeanza rasmi ziara ya kutembelea wanachama wake wa visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba).
Katika ziara hii, Mratibu THRDC, Bw. Baitani Mujuni ameongozana na Afisa Programu wa THRDC Zanzibar, Bi.
Shadida Omar na Afisa dawati la wanachama THRDC, Bi. Lisa Kagaruki.
Ziara hii ina nia kuu ya kumtambulisha Mratibu Zanzibar kwa wanachama, kujua hali ya haki za binadamu kwa kisiwa cha Pemba, kutambua na kushuhudia kazi za wanachama, kufahamu mafanikio ya wanachama, na kufahamu changamoto zinazowakabili wanachama wake kwa nia ya kuzitatua kwa pamoja, na kuwakumbusha wajibu na majukumu yao kama wanachama wa Mtandao. Katika ziara hii, wanachama watapata wasaa wa kushauri Mtandao mambo mbalimbali yanayohusu ustawishaji wa eneo la uanachama.
Ziara imeanza rasmi Pemba, na leo timu ya Mtandao imefanikiwa kutembelea mashirika saba, ambayo ni;
1) Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu kwa Watoto Pemba (JUMAEWAPE)
2) Tusishindwe Development Organization Pemba (TUDOPE)
3) The Popular Inspiring and Relief Organization (PIRO)
4) Chakechake Paralegal Organization (CHAPO)
5) Jumuiya ya Wasaidizi wa Kisheria Pemba (JUWASPE)
6) Pemba Association for Civil Society Organizations (PACSO)
7) Tushinde Development Organization (TUDO)
Kwa jumla wake, THRDC Zanzibar imeona kwamba wanachama wengi waliotembelewa wanafanya kazi kubwa sana kwa jamii ya Pemba, na Zanzibar kwa ujumla.
Imetolewa:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - Zanzibar
29 Agosti 2023.