SIFA NA VIGEZO VYA UANACHAMA
Vigezo vya uanachama wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu kama vilivyowekwa na mkutano mkuu wa mtandao ni kama ifuatavyo:
- Mwanachama ni lazima awe shirika au taasisi adilifu, lililosajiliwa kisheria na sifa zinazotambulika.
- Shirika litakalokuwa tayari kuchangia katika kuendeleza mazingira mazuri na salama kwa Utetezi wa Haki za Binadamu ili kufikia malengo ya Mtandao ya kuwalinda na kuwatetea watetezi wa Haki za Binadamu.
- Taasisi ambayo kazi zake za Utetezi wa Haki za Binadamu zinajulikana na ana moyo wa kuendelea kutetea haki hizo.
Katika maombi shirika liambatanishe vifuatavyo:
- Katiba ya Shirika na cheti cha Usajili.
- Malipo ya ada ya kiingilio ambayo ni Tshs 50,000 (utume risiti ya malipo). Malipo haya hayawezi kurudishwa kwa muombaji (non-refundable)
- Wasifu wa Mkurugenzi wa Shirika (CV).
- Ripoti ya mwaka ya kazi za Shirika.
ADA:
Ada ya kiingilio ni shilingi ……… Tshs. 50,000/=
Pesa zilipwe kupitia;
Account ya Mtandao ya CRDB BANK PLC
Akaunti Namba: 0150408227700
Jina la Akaunti: Tanzania Human Rights Defenders
Branchi: CRDB, Vijana Branch
Account ya Mtandao ya CRDB BANK PLC
Akaunti Namba: 0150408227700
Jina la Akaunti: Tanzania Human Rights Defenders
Branchi: CRDB, Vijana Branch
Na kopi ya risiti kutumwa hapa membersaffairs@thrdc.or.tz.
Shirika litakalokubaliwa kuwa mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Litashiriki katika yafuatayo:
- Ulipaji wa ada yam waka kwa Mtandao, Tsh 100,000 Tu kwa mwaka.
- Kupatiwa taarifa za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu.
- Machapisho ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu.
- Mafunzo mbalimbali yakiwemo ya Usalama wa Watetezi wa Haki za Binadamu.
- Ulinzi na Utetezi pale wanapokuwa katika hali hatarishi au kufunguliwa kesi za kubambikiziwa.
- Mwanachama anapaswa kuhudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa Mtandao (kwa gharama zake binafsi) na mikutano mingine inayoweza kujitokeza kwa kualikwa na Mtandao.
NB: kupatiwa ulinzi ukiwa unafanya kazi ya utetezi na sio kwaajili ya kuhudhuria mikutano tu.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu unatoa mwaliko kwa shirika lolote lenye sifa kuomba uanachama ili kuchangia katika kukuza na kulinda Haki za Watetezi wa Haki za Binadamu Hapa Nchini.