WIKI YA AZAKI 2022: Maendeleo ya Watu, Stori za Watu

WIKI YA AZAKI 2022: Maendeleo ya Watu, Stori za Watu

Mtandao wa Watetezi Wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unashiriki katika wiki ya Asasi za Kiraia nchini Tanzania inayofanyika Arusha.

Wiki ya AZAKI imeanza rasmi leo tarehe 24 Oktoba 2022 ikiwa na malengo makuu ya kuimarisha mahusiano kati ya wadau muhimu wa kimaendeleo.

Dhima ya wiki hii ya AZAKI ni “Maendeleo ya Watu, Stori za Watu”. Hii inaenda pamoja na maonyesha ya kazi mbalimbali za wadau wa maendeleo nchini na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Imetolewa na:
Afisa Habari THRDC
24 Oktoba 2022