WANACHAMA WA MTANDAO WAWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA NA SHERIA YA MTOTO NA. 21 YA MWAKA 2002(OUTREACH PROGRAM OF LEGAL EDUCATION).

Tunduru Paralegal Centre (TUPACE), mwanachama hai wa Mtandao, yaifikia jamii na kutokomeza masuala ya ukatili wa Kijinsia na Haki ya Mtoto kupitia Sheria ya Mtoto ya Mtoto Na.21 ya mwaka 2009, inaendelea kujikita zaidi kwa kuwekeza nguvu kwenye kutoa elimu ya sheria katika Shule za Msingi na Sekondari.

Mkakati wa TUPACE katika Robo hii ya Jan-March, 2022 imedhamiria kuzifikia shule za Sekondari na Msingi zipatazo 18 katika Elimu ya Sheria kwa Program yake ya Upatikanaji Haki (Access to Justice Program). Kupitia timu ya TUPACE iliyojipanga kuzifikia shule hizo 18, tarehe 07 Februari 2022 Mkurugenzi wa TUPACE, Bw.John Nginga aliambatana na watoa huduma msaada wa kisheria, Bw. Yusuph Mbwana (Mratibu) na Bw.Seleman Ally (Afisa Ufuatiliaji na Tathmini) na kufanikiwa kutoa elimu ya sheria katika shule 5. Shule hizo ni za Sekondari Namwinyu, Ligunga Sekondari, Shule za Msingi Namwinyu, Shule ya Msingi Namakungwa pamoja na Shule ya Msingi Ligunga.

Aidha, Mpango huo mahususi unaolenga kuwekeza zaidi elimu kwa vijana mashuleni kuhusu masula ya upatikanaji haki na kulinda ustawi wa haki za watoto pamoja kupinga ukatili wa kijinsia umeendelea kupata ushirikiano mkubwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) Tunduru, Afisa Elimu Msingi na Sekondari, Walimu wa Wakuu wa shule zilizo katika program katika kipindi cha robo hii pamoja na maafisa Watendaji wa Kata na Waratibu Elimu Kata kwa kuhakikisha zoezi linafanyika kama ilivyopangwa.

Jitihada hizi zinalenga pia kupunguza masuala ya kimila yaliyopitwa na wakati hususani masuala unyago kufanyika kwa watoto wa kike wenye umri mdogo wa umri kuanzia miaka 4 hadi 12.

Mwisho, Elimu hii inaambatana na Ushauri kwa watoto wa kike kutoa ushirikiano kwa Viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, Jeshi la Polisi, Wenyeviti wa serikali za Mtaa, Watendaji wa Kata na Mashirika yanayofanya Utetezi wa Haki za Watoto ikiwemo TUPACE.

#Miaka10YaTHRDC
#10YrsOfTHRDC