THRDC YAONGEZA MKATABA WA KUENDELEA KUFANYA KAZI NA AMERICAN BAR ASSOCIATION

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeongeza mkataba wa miezi mitano  wenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu hamsini ( $50,000)  sawa na  Shilingi za Kitanzania Milioni mia moja kumi na sita (Tsh 116,000,000) na Shirika la American Bar Association kutoka inchini Marekani ikiwa ni sehemu ya miradi yake ya kuboresha hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu nchini.  

Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi tarehe 30/10/2022 na Utekelezaji wake utaanza rasmi 01/11/2022 na kumalizika 31/03/2023

Fedha hizi zitatumika kuboresha, hali ya utetezi wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuendeleza kazi za taasisi katika utoaji mafunzo mbalimbali  kwa watetezi wa haki za binadamu nchini.

Shirika la American Bar Association  limekuwa likishirikiana  THRDC tangu mwaka 2020 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya mtandao wakiwa ni Wadau wakubwa wa Haki za Binadamu nchini Tanzania.

Imetolewa na THRDC
4/11/2022