MWANACHAMA WA MTANDAO AWASILISHA MADA KUBITIA TBC TAIFA

Paul Kennedy Makoe – Mkurugenzi Mtendaji wa Community Hands Foundation, ambao ni moja wa mwanachama wa Mtandao awasilisha mada kupitia TBC Taifa leo.

Mada ya: Mchango wa Asasi za kiraia katika maendeleo ya jamii na haki za kibinadam Tanzania.

Bw. Makoe alizungumzia umuhimu wa wa ulinzi na kuheshimu haki za binadamu, pamoja na kuelimisha jamii juu ya athari za uvunjifu wa haki za binadamu.
Jamii kupitia shirika la Community Hands Foundation ilielimika juu ya namna shirika hilo linafanya kazi mbali mbali za kijamii ili kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

Community Hands Foundation limejikita zaidi kwenye
> Kuboresha ustawi wa jamii kwa kuongeza uwezo wa ujasiriamali.
> Kuhakikisha afya njema ya jamii kwa kuanzisha miradi ya afya inayoheshimika na kusaidia jamii.
> Kukuza elimu bora, usawa wa kijinsia kwa jamii na uendelevu.

#Miaka10YaTHRDC
#10YrsOfTHRDC