MKUTANO WA MWAKA WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KILIMANJARO

Leo tarehe 6 Julai 2023, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umehudhuria mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa mkoa wa Kilimanjaro.
Mkutano huu umefuatia mikutano ya mikoa kadhaa juu ya nia ya kuimarisha sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania.
Mgeni rasmi katika mkutano huu ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Nurdin Babu. Wageni wengine waliohudhuria mkutano huu ni wawakilishi na viongozi wa NaCoNGO, wakurugenzi wa NGOs mbalimbali, wawakilishi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), wawakilishi wa mabenki n.k
Katika ufunguzi wa mkutano huu, Mh. Nurdin Babu aeleza kuwa mkoa wa Kilimanjaro una jumla ya mashirika 443 yaliyosajiliwa. Awapongeza ya kuwa mkoa huu umekusanya zaidi ya Bilioni 6.2 za kitanzania, kutoka mashirika 110 tu. Mheshimiwa mgeni rasmi awasisitiza mashirika ya mkoa wa Kilimanjaro kutii sheria bila shuruti ili kuleta matokeo chanya ya mkoa.
Imetolewa na:
Mtandao wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tanzania.