Leo machi 19 THRDC imeshairiki katika kikao kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa mkataba wa Africa wa Haki za Binadamu na watu pamoja na itifaki ya Haki za wanawake Africa.
Kikao hiki kinafanyika Mkoani Dar Es Salaam kwa siku tatu kuanzia tarehe machi 19-21, 2025 ambapo Mgeni rasmi katika kikaohicho alikuwa alikuwa waziri wa katiba na sheria Mheshimiwa Damas Ndumbaro akiambatana na Mkurugenzi msaidizi idara ya haki za binadamu kitengo cha utoaji taarifa Bi. Beatrice kitengo, makamu wa Tais wa TLS Bi. Letitia Mtagazwa na Dr Deus Mkiza mwakilishi wa jukwaa la habari la wahariri Tanzania.
Mheshimiwa Waziri katika kutoa hotuba yake alizungumzia Kuwa serikali imeona umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wahabari, CSOs, watu wenye ulemavu na wadau wengine wa masuala ya haki za binadamu kote Tanzania bara na Zanzibar katika mchakato huu muhimu wa kupitia rasimu ya taarifa ya nchi ya utekelezajiw wa mkataba wa Africa wa haki za binadamu na watu ( ACHPR) na itifaki ya haki za wanawake Africa.
Aliekeza kuwa Tanzania inatekeleza maagizo ya mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu na sheria za nchi kwa kupitia 4Rs ambayo hii imekuwa Falsafa ya Mheshimiwa Rais wa awamu ya Sita Dr. Samia Suluhu Hassani.
Mh. waziri alisema wazi kuwa yapo mambo mengi ambayo tukiyaangalia yanaonyesha utekelezwaji wa haki za binadamu nchini yakiwemo;
• uwepo wa ibara za haki za binadamu katika katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ( Bills of rights)
• Tume ya haki za binadamu na utawala bora
• usaji na uwepo wa asasi za kiraia nchini,
• nchi ku saini na kuridhia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu,
• Uwepo wa mhimili wa mahakamana uhuru wake katika kutoa maamuzi,
• uwepo wa mahakama za kimataifa za haki za binadamu nchini kwetu,
• Utoaji wa taarifa za utekelezaji wa haki za binadamu nchini,
• Kuundwa kwa mama samia legal aid kampeni na vingine vingi.
Alisisitiza kuwa mapitio haya yatazingatia katika kuangalia haki zote zikiwemo haki za kiuchumi, kiraia, kijamii, na za kisiasa kwa muktadha wa Tanzania na Africa na kuepuka kuangalia na kutafsiri haki za binadamu kwa muktadha wa kimagharibi bila kusahau kuangalia wapi tulipotoka, tulipo na tunapokwenda. Tukionyesha wapi tumefanya vizurii na wapi panahitaji maboresho na maboresho pia.
Aliongeza kuwa nchi yetu iruhusu watu kuishi sehemu yoyote kulingana na sheria za nchi, na iko wazi kuwa sheria zetu za ardhi hazijatoa kibali cha umiliko wa ardhi ( no right of ownership of land but only occupancy or lease) hivyo basi pale inapoona wananchi wanaishi katika maeneo hatarishi kama maeneo ya hifandhi ambapo ni hatarishi kwa usalama wa haki ya kuishi kwa matukio kama kuuawa na wanyama wa hifadhi, au ukosefu wa huduma za kijamii katika maeneo hayo, serikali inalojukumu la kuwahamisha na kuwapeleka sehemu salama kwa maslahi yao na maslahi ya umma kiujumla.
Alimaliza kwa kusema faida ya ujumuishwaji katika kupitia taarifa hizi za utekelezaji wa haki za binadamu nchini na kuwa na ripoti jumuishi ni kwa lengo la kukuza uwazi, Uwajibikaji kwa serikali na wadau wote, kukuza maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kuwasaidia wahanga wa ukiukwaji wa haki za Binadamu na ukatili wa kijinsia.
THRDC 19 MACHI 2025
