MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MTANDAONI NA WAHARIRI KUHUSU UZINGATIAJI WA SHERIA NA KURIPOTI MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU

Morogoro, Tanzania

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na taasisi ya International Center for Not-for-Profit Law (ICNL) wanatoa mafunzo kwa waandishi wa habari za mtandaoni na wahariri juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria zinazosimamia tasnia ya habari pamoja na kuripoti matukio ya haki za binadamu nchini Tanzania.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika mjini Morogoro na yanalenga kuwajengea uelewa waandishi wa habari za mtandaoni na wahariri kuhusu sheria zinazowaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha kupitia mafunzo haya, waandishi wa habari wataweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari na kupendekeza namna bora ya kuzitatua kwa kushirikiana na wadau, asasi za kiraia na serikali.