MAFUNZO KWA ASASI ZA KIRAIA TANZANIA NAMNA YA KUEPUKA UTAKATISHAJI WA FEDHA NA UFADHILI WA MIPANGO YA KIGAIDI

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), wakishirikiana na Taasisi ya Haki za Binadamu Afrika Mashariki (EAHRI) na Shirika Lisilo la Kiserikali Defenders Protection InternationaI (DPI) lenye Makao yake Nchini Uganda wameandaa Mafunzo ya Siku 2 yatakayofanyika Dar es salaam kuanzia Tarehe 13/03/2023 hadi 14/03/2023.


Malengo  ya mafunzo haya  ni mengi, yote yanajumuishwa katika malengo makuu yafuatayo:


1. Ni kuzifahamisha Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kiserikali nini maana ya utakatishaji fedha, njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kutakatisha fedha kupitia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kiserikali na fedha ambazo zinapatikana na kutumika kufadhili ugaidi, na jinsi gani utakatishaji fedha unatokea .

2. Jinsi gani Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kisirikali zinaweza kutokomeza kabisa utakatishaji fedha nchini Tanzania na ufadhili wa mipango ya kigaidi.

3. Kuzijengea uwezo asasi za kiraia jinsi ya kuepukana na fedha na mali zilizopatikana kwa njia haramu na zenye lengo la kufanyiwa utakatishaji au kufadhili ugaidi. 

4. Kuwajengea uwezo AZAKI/Watetezi wa haki za binadamu juu ya sera, sheria na mikakati inayoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania ili kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi hasa kwa upande wa mashirika yanayofanya kazi bila faida (NPOs/AZAKI) 

5. Kuhakikisha mikakati hii mizuri ya kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi haitumiki vibaya kwa malengo yasiyo rasmi  kudidimiza nafasi za kiraia nchini ( Civic Space) 


Washiriki wanaoshiriki kwenye mafunzo haya ni wawakilishi  toka ofisi za wasajili wa AZAKI nchini (toka Ofisi ya Msajili NGOs na Mrajis wa AZAKI toka Zanzibar.  Wengine ni wataalam toka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya ndani (Toka Idara  Maalum ya kudhibiti Fedha Haramu -FIU), Baraza la NGOs (NACONGO), Asasi za Kiraia na watetezi wa haki za binadamu.