JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI DAR ES SALAAM.

"Msisitizo wangu ni kwamba kama tumesajiliwa na tunafanya kazi chini ya sheria basi ni vizuri pia sheria hizi hizi zikaendelea kuakisiwa vizuri katika utumishi wetu na ninafikiri pia mashirika yote yasiyo ya serikali usajiri wake na malengo yake huwa zinaangalia mahitaji yaliyopo katika jamii, na zile fursa zilizopo kuna ambazo zimejikita katika elimu, mazingira, afya na ukatili wa kijinsia maana vitu vyote hivi ni fursa, kuna utafiti ambao nimeufanya na kuona kwamba kuna pengo kitu ambacho kitasaidia serikali kuziba ilo pengo ni kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali ili tuweze kwenda mbele zaidi sasa haya yote ambayo mmeyaangalia ni vizuri basi yakaendelea kutekelezeka na hapo baadae mnapokuja kufanya monitoring evaluation mnaweza kugundua kama mmefanya kazi nzuri au kazi ambayo haijawa na matokeo mazuri." Mhe- Albert Chalamila.