JUKWAA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI SINGIDA

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unashiriki katika jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Singida linalofanyika leo tarehe 03 na 04 Julai 2023. Jukwaa hilo lililoandalia na Baraza la Kitaifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Singida (NaCoNGO - Singida) linayaleta pamoja mashirika mbalimbali Tanzania ikiwemo mashirika wanachama wa Mtandao waliopo mkoani Singida na wadau muhimu kutoka sekta mbalimball kama vile taasisi binatsi, taasisi za kiserikall, mashirika yenyewe, watanyabiashara, wajasiriamali, na walezi wa mashirika hayo ambao ni wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu.
Katika siku hizi mbili, masuala ya kustawisha maendeleo ya mashirika yatajadiliwa, ikiwemo mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akihutubia jukwaa hilo, Mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Peter Serukamba amesema serikali inatambua umuhimu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika mendeleo ya nchi. Serukamba amesema mbali na mashirika hayo kufanya kazi nzuri ameyataka kufuata katiba, kanuni, miongozo ya serikali.
Naye wakili Onesmo Olengurumwa Mratibu kitaifa wa THRDC amesema asasi za kiraia ni moja ya sekta tatu kubwa duniani zinazochangia katika maendeleo ya nchi yoyote ile.
THRDC inaendelea kujenga na kuimarisha taasis ili ziweze kuwa chachu ya Maendeleo ya Taifa letu.
Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.