MIAKA 10

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) leo hii Mei 13, 2022 unaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2012.


Maadhimisho haya yanaadhimishwa sambamba na kipindi cha hafla ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa kuwepo madarakani kwa Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.


Sherehe za maadhimisho haya zinafanyika katika Ukumbi wa PSSSF, Jijini Dar es Salaam, zimehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka taasisi za kitaifa na kimataifa, ikiwemo mabalozi,  mawaziri mbali mbali, makatibu wakuu kutoka katika Wizara mbali mbali, viongozi wa kidini, kisiasa, taasisi za kimataifa za utetezi wa Haki za Binadamu Afrika, majaji, Mawakili, wanachama wa Mtandao wa Haki z Binadamu Tanzania pamoja na waandishi wa Habari.


Katika maadhimisho hayo Mtandao unatarajia kuzindua Ripoti inayoonyesha kazi za mtandao huo kwa miaka 10, Ripoti ya hali ya watetezi wa Haki za Binadamu kwa mwaka 2021 pamoja na kumtunuku tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa namna amefanikiwa kusimamia Haki za Binadamu katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha mwaka mmoja aliokuwepo madarakani.


Hafla hii pia itaambatana na utoaji wa vyeti vya shukrani kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamekuwa bega kwa bega na mtandao Kwa kipindi cha miaka 10 ulipokuwa ukifanya kazi na Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania. 


Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania umeendelea kufanya kazi Kwa ukaribu na Watetezi wa Haki za Binadamu zaidi ya 200 Nchini Tanzania bara na visiwani na kuweza kufikia maelfu ya watanzania katika kulinda kutetea na kuendeleza Haki za Binadamu Nchini. 


Sherehe za Maadhimisho yote haya zipo mubashara (live) katika Ukurasa wa You Tube wa Watetezi TV, Dar Mpya, IKULU mawasiliano pamoja na vyombo mbali mbali vya habari Nchini.


Bofya link Kutazama https://youtu.be/6Rg6z87rUfo. (WATETEZI TV)


https://youtu.be/u3dTBGexnpk (DAR MPYA)


Hashtags

 #Miaka10yathrdc

#10yearsofthrdc

#Adecadeofthrdc


MITANDAO YETU

Instagram @thrdcoalition @watetezitv

Twitter @THRDCOALITION @watetezitv


Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

Mei 13, 2022