Leo tarehe 23/6/2024 wadau kutoka sekta mbalimbali nchini Tanzania wamekutana jinini Dodoma kwa lengo la kutoa maoni yao na mapendekezo juu ya mswada wa Fedha wa mwaka 2024 - (Financial Bill 2024)
THRDC ikiwakishwa na Mratibu wa Mtandao wakiliOnesmo Olengurumwa, Ndugu Musa Jonasi - Mwakilishi wa katibu Nacongo na Ms. Charlotte Kabunga - mwakilishi THRDC kanda ya kati wameipongeza Wizara ya fedha kwa kukubali baadhi ya mapendekezo ya AZAKI ya muda mrefu kuhusu kurekebisha kifungu cha 64 cha Sheria ya Mapato ya Kodi kwa kupanua tafsiri ya Shirika la Hisani ( charitable organization) na kuongeza tasisi za afya na mazingira katika tafsiri hiyo kwani ni hatua nzuri .
Katika kuwasilisha Mapendekezo ya maboresho ya mswada huo Wakili Olengurumwa Aliiambia kamati kuwa mabadiliko hayo bado ni madogo sana ukilinganisha na mapendekezo ya AZAKI ambayo yamekuwa yakitolewa kuitaka tafsiri hiyo iguse maeneo yote yanayofanyiwa kazi na AZAKI kama vile Eneo la utoaji wa msaada wa kisheria, eneo la utoaji elimu ya kupingana na ukatili kwa wanawake na Watoto, haki za binadamu na utawala bora nakadhalika.
Pia anapendekeza kamati ya maboresho ya sheria ya kodi iwe jumuishi kwa kuwa na mwakilishi/wawakilishi kutoka AZAKI ili kuhakikisha hoja zao zinawasilishwa na kwa ajili ya kuongeza maboresho katika sheria ya kodi kwani inayowagusa kwa namna moja au nyingine.
Mwenyekiti wa kamati aliyapokea mapendekezo hayo yaliyowasilishwa pia kwa njia ya maamdishi na kuahidi kuwa yatafanyiwa kazi, aliwakumbusha wadau kuwa uongozi wa awamu hii umeipa sana kipaumbele Secta ya AZAKI kwani imewatengea wizara maalumu ya maendeleo ya jamii na pia kianzisha kamati maalumu ya bunge ya maendeleo ya jamii, haya yote imaonyesha umuhimu wa secta hii ya AZAKI katika Kukuza maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
IMETOLEWA NA THRDC
23 June 2024