Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umesaini mkataba wa mwaka mmoja (1) wenye thamani ya Euro laki moja na themanini na shirika la Protection International Afrika
Mkataba huu wa mwaka mmoja umelenga kusaidia kukuza nafasi ya kiraia nchini kwa kuimarisha ushiriki wa Makundi yote ya Watetezi wa Haki za binadamu (USAWA). Shughuli zitakazotekelezwa kwenye mradi huu zitachangia moja kwa moja kwenye kutekeleza malengo ya Mpango mkakati mpya wa Mtandao (2023- 2027)
Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi leo April 14, 2023 na utekelezaji wake utaanza mapema mwezi huu na kumalizika December 31, 2023. Mojawapo ya wanufaika wa mradi huu ni Watetezi wa Haki za Binadamu bara na visiwani, wakiwemo watetezi wa haki za wanawake, watu wenye ulemavu na jamii za kifugaji. Mradi huu unatarajiwa kuongeza nguvu katika utetezi wa haki za binadamu nchini kwa kuboresha mazingira yenye usawa kwa jamiii nzima.
Imetolewa na THRDC,
April 14, 2023