Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesaini mkataba wa miaka minne wenye thamani ya USD 600,000 na Wellspring Philanthropic Fund (WFP) kwa kipindi cha mwaka 2024-2027. Mkataba huu mpya umejengwa juu ya muongo mmoja wa ushirikiano wenye mafanikio na WFP na unalenga kusaidia kwa ujumla kwenye utekelezaji wa Mpango Mkakati wa THRDC wa (2023-2027) wenye malengo makuu yafuatayo:
1 Kuwajengea Uwezo Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
2 Kufanya Shughuli za Uchechemuzi na Ushirikishwaji
3 Kutoa Ulinzi kwa Watetezi wa Haki za Binadamu
4 Kuimarisha na Kuendeleza Taasisi
Utekelezaji wa mkataba huu utaanza rasmi Septemba 2024 na utaendelea hadi Oktoba 2027. Wanufaika wa mradi huu ni Watetezi wa Haki za Binadamu wa Tanzania Bara na Zanzibar. THRDC inashukuru kwa msaada endelevu wa WFP na ina matumaini kuwa mradi huu utaongeza nguvu zaidi katika kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ya Watetezi wa Haki za Binadamu na kazi ya utetezi wa Haki za Binadamu nchini kwa ujumla.
Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Tarehe: Julai 29, 2024