THRDC YAKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA UBALOZI WA JAPAN

Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC, hii leo umefurahi kupata ugeni wa kiongozi wa kitengo cha maswala ya Siasa, Utamaduni na Mahusiano ya Umma kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania Bi. Ogawa Eri.

Bi Ogawa ambaye ameutembelea mtandao leo April 19, 2022 amekutana na Mratibu kitaifa wa Mtandao wa THRDC, Bw. Onesmo Olengurumwa na kujadiliana namna ya kujenga, kukuza na kuboresha mahusiano kati ya THRDC na ubalozi wa Japan. Katika mazungumzo hayo mratibu THRDC amemkaribisha Bi Ogawa katika maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao yanayotarajia kufanyika Mei 13, 2022.

THRDC imekuwa ikishirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo balozi mbali mbali, wadau wa maendeleo katika kuhakikisha wanashirikiana na mtandao kupelekea mbele ajenda mbali mbali za watetezi wa Haki za binadamu nchini hatua ambazo zimeisaidia zaidi sheta ya utetezi wa haki za binadamu nchini. THRDC inaamini mkutano huu ni mwanzo mzuri wa mashirikiano baina na THRDC na ubalozi wa Japani pamoja na mwendelezo wa mashirikiano baina yake na wadau wengine wa maendeleo Nchini.

#10yearsofthrdc
#Miaka10yathrdc

Imetolewa na Afisa Habari THRDC
19 May, 2022