THRDC IMESAINI MKATABA WA RUZUKU NA PACT

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesaini mkataba wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Tatu na Laki Saba (Tsh. 23,700,000) na PACT.Mkataba huo unalenga kusaidia na kuimarisha shughuli za haki za binadamu nchini Tanzania.

Mkataba huo ulitiwa saini rasmi tarehe 19 Aprili 2022 na utekelezaji wake utakamilika tarehe 30 Aprili 2022.

Fedha hizo zitatumika kusaidia shughuli za watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. Pia katika kuimarisha kazi za watetezi wa haki za binadamu zikiwemo Asasi za Kiraia na Waandishi wa Habari kupitia mikutano ya mazungumzo na serikali na wadau wengine wa haki za binadamu nchini.

PACT ni moja ya Wadau wakubwa wa THRDC na Mdau wa Haki za Binadamu nchini Tanzania.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
20 Aprili 2022