Juni 23 2024. Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu - THRDC umeweza kufanya ziara katika Gereza la vijana Wami lililopo mkoani Morogoro Dumila kukabidhi Magodoro Takribani 30 na vifaa vya michezo kwa ajili ya vijana katika gereza hilo.
Gereza hilo limeanziahwa mwaka 1968 kama taasisi ya uboreshaji vijana ambalyo ni taasisi Pekee na kituo kinachotoa mafunzo ya fani zaidi ya 7 ikiwemo fani ya Umeme, Useremala, Uashi/Ujenzi, ushonaji, ufundi bomba, uchomeleaji na ufundi makenika kwa vijana waliokinzana na sheria.
Akizungumza na kamishima msaidizi wa magereza Abdala Hassan Missana ambae ni mkuu wa taasisi hiyo, Mratibu wa Mtandao wakili Onesmo Olengurumwa alisema kuwa ziara hii ni imelenga kukabidhi vifaa hivi kwa vijana Hawa wafungwa kama moja ya jitihada za kujakikisha hata wafungwa wanapokuwa katika magereza wanapat haki zao za msingi za binadamu na kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Akisisitiza juu haki za binadamu kwa wafungwa magerezani , wakili Olengurumwa alisema ni jukumu la serikali kuboresha miundombinu katika Magereza haya na wadau mbalimbali kusaidia upatikanaji wa mahitaji Ya kijamii ili kulinda ma kudumisha haki za binadamu kwa wote na maeneo yote.
THRDC
24 June 2024