MAFUNZO KWA VIONGOZI WAPYA WA KANDA WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)

Dodoma, Tanzania

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) leo wameendesha warsha ya siku mbili kwa viongozi wapya wa kila kanda ya Chama hicho cha Mawakili Tanganyika (TLS Chapter leaders). Warsha hii iliyoanza leo tarehe 20 Mei 2021jijini Dodoma katika ukumbi wa African Dream Hotel inatarajiwa kukamilika kesho tarehe 21 Mei 2021.

Warsha hii inajumuisha mafunzo kuhusu kesi za haki za kibinadamu na kesi za kimkakati. Viongozi wa kikanda watapokea mafunzo kuhusu fursa na taratibu za kimahakama katika kutetea haki za kibinadamu kupitia kesi za kimkakati. Vilevile mafunzo haya yanalenga kuwafundisha na kuwajengea uwezo viongozi hawa jinsi ya kuogonza kanda zao. Miongoni mwa wawasilishaji katika mafunxo haya ni Mh. Jaji mstaafu Robert Makaramba.

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Mei 20, 2021