KUKAMATWA KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU, NA WAKOSOA MKATABA WA BANDARI.

 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Jukwaa la Katiba Tanzania kwa pamoja tunalaani kukamatwa kwa Wakili Boniface Mwabukusi pamoja na wakosoaji wa Mkataba wa Bandari chini ambao ni Dr. Wilbroad Slaa na Mpaluka Said Nyagali. Mawakili wa watuhumiwa hao wametueleza kwamba tuhuma zinazowakabili ni kosa la uhaini ambapo wamehojiwa
kwa nyakati tofauti katika vituo vya Polisi.