JUKWAA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KIGOMA.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeshiriki katika jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma. Jukwaa hilo lililoandaliwa na Baraza la Kitaifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kigoma (NaCoNGO - Kigoma) limefanyika kwa muda wa siku tatu, Agosti 2 - 4, 2023. Huku likileta pamoja wawakilishi wa mashirika mbalimbali Tanzania ikiwemo mashirika wanachama wa Mtandao waliopo kanda hiyo, na wadau muhimu kutoka sekta mbalimbali.
Katika siku hizo tatu, masuala ya kustawisha maendeleo ya mashirika yamejadiliwa, ikiwemo mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali. THRDC kupitia Wakili Paul Kisabo ambaye ni muwakilishi wa Mratibu Kitaifa, imeelimisha wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKi) kwenye jukwaa hili juu ya Uwajibikaji na ufuataji wa sheria na sera zinazoongoza mashirika yasiyo ya kiserikali, ikiwemo masuala ya utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi. Mgeni rasmi katika jukwaa hili alikua mkuu wa mkoa wa Kigoma,
Mhe. Cgf (Rtd) Thobias E. Andengenye.
Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.