Shirika
la linaloshughulika kutetea haki watetezi wa haki za binadamu Afrika
(DefendDefenders), Kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za
Binadamu Tanzania (THRDC), wanafanya warsha ya kuhusu nafasi za kiraia
na haki za binadamu.
Warsha hiyo imeanza leo Desemba 7, hadi
Desemba 10, 2022, ikifanyika kwenye ukumbi wa Giraffe Hotel jijini Dar
es Salaam, na kuhudhuriwa na watetezi @euintanzania wa haki za binadamu kutoka mashirika wanachama wa THRDC, CWHRD na wadau mbalimbali.
Katika
warsha hiyo ya siku nne, wadau hao wanatarajiwa kutumia fursa hiyo
kujadili hali ya mazingira ya utetezi wa haki za binadamu nchini pamoja
kuwapatia stadi mbalimbali watetezi hao ambazo zinaweza kuwasaidia
kukabiliana na changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo.
Aidha
siku ya mwisho ya Warsha hizo zinazofanyika mfululizo inatarajiwa
kuhitimishwa kwa maadhimisho ya Siku Kimataifa ya Haki za Binadamu
pamoja na kuhitimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
huku viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wadau wa haki za binadamu
zaidi ya 200 wakitarajiwa kuhudhuria.
#ClaimingSpacesTz22
Imetolea na
THRDC
