ZIARA YA MRATIBU THRDC NA AFISA DAWATI LA WANACHAMA YAINGIA SIKU YA TATU MKOANI ARUSHA

Ziara ya siku tatu ya Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Ndugu Onesmo Olengurumwa akiongozana na Mratibu Msaidizi wa THRDC Kanda ya Kaskazini Bwana Erick Luwongo pamoja na Afisa wa Dawati la Wanachama – THRDC Wakili Joyce Eliezer inaendelea leo mkoani Arusha kwa kutembelea mashirika wanachama wa THRDC.

Kwa siku ya leo Mratibu na timu yake wameanza kwa kulitembelea shirika la TNRF (Tanzania Natural Resource Forum) na baadaye Haki Madini na PINGOs Forum.

[envira-gallery id=”5863″]

Shughuli kuu katika ziara hii ni kufanya mazungumzo na Mashirika Wanachama wa THRDC kuhusu fursa na changamoto katika utetezi wa Haki za Binadamu nchini.

Tangu kuanza kwa ziara hii siku ya Jumanne tarehe 11 Februari 2020, tayari mashirika manne ya CiLAO (Civic and Legal Aid Organization, TAWLA, HakiKazi Catalyst na LHRC yameshatembelewa.

Siku ya kesho ziara hii itaendelea katika Mkoa wa Kilimanjaro na hatimaye Mkoani Tanga.

Imetolewa na:
Dawati la Wanachama THRDC
Februari 14, 2020