Mratibu kitaifa waMtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania Onesmo Olengurumwa hii leo ametembelea taasisi ya Mwanza Press Club, Taasisi Mwamvuli wa waandishi wa Habari inayosimamia utendaji wa Kazi za waandishi wa Habari kwa mkoa wa Mwanza.

“Tunaamini waandishi wa Habari hawawezi kufanya kazi binafsi bila kuwa na chombo kinachowasimamia pindi wanapokumbana na changamoto mbali mbali hvyo Taasisi ya MPC imekuwa ikiwapatia waandishi mafunzo mbali mbali yanayowajengea uwezo wa kuendana taratibu na sheria zinazosimamia utendaji wa vyombo vya Habari, lakini pia tunashukuru sana THRDC kwani imekuwa mstari wa mbele kuisaidia taasisi pale ambapo waandishi wanapokumbana na matatizo mbali mbali, changamoto za kisheria kwa mfano mwandishi mwenzetu Albert Sengo alipopata changamoto akiwa kazini THRDC iliingilia kati kumsaidia, n ahata waandishi wengine hata taasisi yetu ya MPC pindi inapokubwa na matatizo mbali mbali THRDC imkeuwa mstari wa mbele kutusaidia, n ahata sasa kesi nyingine zinaendelea na THRDC kupitia wakili wake Amri Linus amekuwa akitupatia usaidzi wa kisheria na kuwanasua wanachama kwenye changamoto hizo.” Bernad James, Katibu Mwanza Press Club

“Tumekuwa tukiendesha mafunzo ya mtandaoni kwa waandishi wa Habari, tumekuwa tukisaidia waandishi pindi wanapokumbana na changamoto za kijamii kwa kuwafutia msaada kutoka kwa wadau mbali mbali, tumejenga mahusiano mazuri na serikali, taasisi za kifedha, taasisi za kisheria, taasisi za elimu, vyuo mbali mbali, tumekuwa tukiendesha mijadala mbali mbali na wadau na kama jeshi la polisi, lakini pia taasisi mwaka huu iliweza kuandaa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari, ambapo tuliwakutanisha waandishi wa Habari na taasisi kama jeshi la polisi, Mkuu wa mkoa na wadau wengine malengo ni kuweza kujenga mahusiano lakini pia kuwawezesha waandishi wa Habari kuweza kufanya kazi zao katika mazingira mazuri” Anaongeza Bernad James Katibu MPC

Taasisi ya MPC inakiri kuwa msaada kwa waandishi wa Habari hasa katika kuwawezwesha baadhi ya wanachama kutumia vifaa vya taasisi katika utayarishaji wa kazi za kihabari ambazo huandaliwa kwa mwongozo kutoka katika taasisi bure kabisa, hii imewawezesha waandishi kuwa na mazingira mazuri ya ufanyaji kazi Pamoja na uandaaji wa Habari kwa weledi.

“MPC ni taasisi kongwe yenye wanachama Zaidi ya 200, na tumekuwa tukijihesabu kama watetezi wa haki za binadamu, kwani ukiondoa Dar es Salaam, Mkoa wa Mwanza unaweza kuwa wa pili kwa matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu hivyo katika kujengewa uwezo na usaidizi wa mahsauri ya mahaka THRDC imekuwa ikitusaidia karibu kesi zote tulizofungua mahakamani, na hata leo tulikuwa na kesi ambayo THRDC imetpatia wakili na hata kwa kesi nyingie kama za Albert Sengo, Chibuga na wengine, tumekuwa tukipata wasaha wa kuwajengea uwezo waaandishi wa Habari katika maswala ya UVIKO 19 ambapo kwa mara ya Mwisho tulifanikiwa kupata usaidizi wa kukaa na wadau wa Afya ili kujadili kuhusiana na janga hili ambapo THRDC ilitusaidia katika upande wa mitambo.”Edwin Soko Mwenyekiti wa Mwanza Press Club

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Edwin Soko anakiri kuwa bado waandishi wanaishi katika mazingira magumu ya utambuzi wa haki zinazowasimamia katika utendaji kazi, lakini pia kumekuwa na changamoto za kiusalama kwa waandishi wa Habari ambazo mara nyingi huwaweka hatarini pindi wanapofanya nkazi ya ukusanyaji wa Habari mbali mbali zenye maslahi ya watu wachache, uelewa ndogo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na kufahamu namna ya kufanya kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali fedha ili kuweza kujiendesha, na kuiomba taasisi ya THRDC kuona uwezekano wa kuwajengea uwezo waandishi wa Habari katika masuala hayo Pamoja na kuwapatia mafunzo ya usalama ili waweze kuendelea kuwa salama Zaidi katika ufanyaji wa kazi zao, lakini pia waandishi wa habri wanapokuwa wanapata changamoto za kisheria Wamekuwa wakikimbilia kwenye taasisi kama MPC kwa msaada wa kisheria huku waajiri wao wakikaa pembeni na kupelekea taasisi kulemewa na kesi nyingi n ahata kukosa rasilimali za kutosha kusaidia kwa upana Zaidi.

MPC imeiomba Taasis ya THRDC Kuangalia namna ya kuandaa ‘compendium’ ya sheria zinazosimamia vyombo vya Habari ili iweze kuwaongoza waandishi kuzitambua haki zao na hazi zinazowaongoza katika ufanyaji kazi na vyombo vya Habari, lakini pia kuwapatia waandishi vitendea kazi kama Press Jackets ambazo zinaweza kuwatambulisha pindi wanapofanya kazi ya kukusanya Habari katika mikusanyiko mikubwa kama mikutano mbali mbali ya kampeni za kisiasa.

Mratibu THRDC ameishauri taasisi ya MPC kuendelea kuboresha umoja wao kwani katika mitandao hiyo ndipo waandishi wanapata unafuu na usaidizi wa kupata haki zao kwa wakati, lakini pia ameitaka MPC kuendelea kujenga mashirikiano na taasisi nyingine kama ilivyofanya kwa THRDC kwani kupitia hayo fursa nyingi Zaidi huapatikana, kuangalia namna ya kuboresha taasisi, kutengeneza mifumo mizuri ya kuwa imara kuanzia kwenye mashina, lakini hata kuwawezesha wanahabari kuwa imara katika kazi zao, ili kuweza kuvutia wadau ambao wanaweza kuinufaisha taasisi na kuiwezesha kufanya kazi Zaidi. Mratibu THRDC amitaka MPC Kupitia mpango wa miaka mitano wa serikali kwani imetaja sekta ya vyombo vya Habari na kuangalia namna inaweza kufanya kazi kwa kuzingatia malengo yaliyopo kwenye mkakati huo na kuisaidia serikali kutimiza malengo yaliyopo katika mkakati.

Imetolewa Na Mtadao Wa Watetezi Wa Haki Za Binadamu Tanzania Leo
AGOSTI 10, 2021