Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa anaendelea na ziara ya kutembelea wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC ambapo Leo Mratibu ametembelea Shirika la UVUUMA linalopatikana Wilayani Magu mkoani Mwanza.

UVUUMA ni Shirika linalojishughulisha na Kazi za utetezi wa Haki za watoto na watu wenye Ulemavu kwa kuwajengea uwezo wa utambuzi wa Haki zao lakini pia katika eneo laa watu wenye Ulemavu Taasisi imekuwa ikifanya Kazi kwa karibu na Taasisi kama SHIVYAWATA na CHAWATA.

Taasisi ya UVUUMA imekuw aikifanya Kazi katika eneo la watoto hasa wale ambao wamekumbwa na madhila ya kufukuzwa majumbani mwao kwa Sababu mbali mbali Hasa ujauzito.

UVUUMA imefanikiwa kuchochea mabadiliko kwenye jamii hasa katika suala la kupunguza kasi ya matukio ya ukatili wa kijinsia, lakini pia taasisi Inakiri Kuwa hali ya usala ma kwa sasa inaridhisha tofauti na wakati wa nyuma ambao Kazi za utetezi zilikuwa zikitekelezwa kwa shida kuhofia Usalama. Taasisi ya UVUUMA imefanikiwa kujenga ofisi mpya zitakazoliwezesha Shirika kufanya Kazi kwa uhuru na nafasi.

Pamoja na mafanikio hayo taasisi ya UVUUMA inakumbwa na changamoto hasa Baada ya kuzuka kwa ugonjwa wa UVIKO19 ambapo wafadhili wamekuwa wakisitisha miradi, kumekuwa na uelewa mdogo wa wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali juu ya masuala ya Usalama hasa pale miongozo ya taasisi inapotelewa kwa wakurugenzi tu, jambo linalohatarisha uhai wa Taasisi endapo Mkurugenzi hatokuwepo kwenye nafasi hiyo.

Mratibu THRDC ameipongeza taasisi ya UVUUMA kwa kupiga hatua na Kufanikiwa kufanya ujenzi wa Ofisi kubwa zaidi, laamini pia amewashauri wakurugenzi Kuwa na tabia ya kutoa fursa kwa wafanyakazi wa Taasisi kuhudhuria Mafunzo mbali mbali yatakayowaongezea uelewa wa namna taaisi za Haki za Binadamu zinavyofanya Kazi, lakini pia ameitaka taasisi kuzingatia miongozo iliyoandaliwa na THRDC inayowawezesha kufanya Compliance wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

Mwisho Mkurugenzi wa Shirika la UVUUMA Sylivester Kakinda ameushukuru Mtandao na Mratibu kwa kupata wasaha wa kutembelea wanachama na kuyatambua mazingira ya ufanyaji Kazi wa taasisi hizo.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC
11/08/2021