Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa akiongozana na Afisa dawati la wanachama Bi Lisa Kagaruki, Pamoja Mratibu wa Kanda ya Ziwa, Bi Sophia Donald wametembelea shirika la Haki Zetu linalofanya kazi mkoani Mwanza ambalo pia Lina matawi mawili, Moja wilaya ya Magu, na lingine mkoa wa Arusha.

Shirika la Haki Zetu linajihusisha na haki za wanawake na vijana mbali mbali wanaokumbana na changamoto mbali mbali katika mkoa wa Mwanza.
Kwa upande wa haki za wanawake, shirika limejikita kwenye Kupinga unyanyasaji wa kujinsia, ndoa katika umri mdogo, Pamoja na mimba katika umri mdogo, Pia shirika hili limekua likitoa elimu ya afya kwa vijana na wanawake.

Hata hivyo Shirika hili limekua likikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo
– Matokeo ya ugonjwa wa UVIKO 19 uliopelekea Kazi nyingi za shirika kushindwa kufanyika kwani taasisi imekuwa
ikihusisha ukusanyikaji wa wadau kujadili changoto mbali mbali zinazomkumba mtoto wa kike Pamoja na utoaji wa Elimu. Gonjwa hili la mlipuko limesababisha usimamishaji wa baadhi ya kazi za shirika huku baadhi ya wafadhili wakiondoka Kutokana na kusimama kwa miradi.
– Taasisi ya Haki zetu imekuwa ikikumbana na Changamoto za kiusalama, hasa kupokea vitisho kutoka kwa jamii, hasa pale ambapo taasisi imekuwa Ikitoa elimu ya afya katika ngazi ya chini na kuhisiwa kuwafundisha watoto mabo yasiyo na maadili.

Kupitia changamoto ya UVIKO 19 taasisi Inakiri kujifunza Kuwa iwapo katika jamii kutakuwa na mtu mmoja ambaye hatokuwa salama basi jamii nzima haitakuwa salama hivyo taasisi imekuwa ikifanya bidii kuhakikisha linatetea Haki za mabinti ma wanawake katika jamii na kuhakikishaa wanakiwa salama. Lakini pia katika kujaribu kutatua changamoto hizi, Shirika la Haki Zetu limekua likitoa elimu kwa jamii juu ya masuala ya haki za binadamu. Elimu hii inatolewa pia kwa njia ya alama ili kuwafikia wahusika wote.

Shirika la Haki Zetu limefanikiwa kuhamasisha na kuwaelimisha sana wanawake na vijana katika ngazi za vijiji, Uhamasishaji wa kiuchumi pia umefanyika, ambapo Haki Zetu imeweza kufundisha ushonaji kwa vijana kadhaa, na nguo zinazoshonwa zinaongeza kipato kwa vijana hao.
Pia shirika linaendesha kampeni ya uelimishaji juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia- GBV kupitia michezo ya mpira kwa vijana, “Piga Chenga Sio Mkeo”.

Mkurugenzi wa Shirika la Haki Zetu ameshurukuru sana kwa mafunzo yaliyotolewa na Mtandao mnamo mwezi Juni 2021. Mafunzo hayo ni pamoja na mafunzo ya usalama, pamoja na mafunzo ya kodi za mashirika yasiyo ya kiserikali lakini pia Amepokea kwa shukrani vitabu vya miongozo vilivyotolewa na Mtandao, na kuahidi kuzitumia katika utekelezaji wa majukumu ya kishirika.

Mratibu THRDC pia alipata wasaha wa kuelezea kwa ufupi juu ya jarida la uwajibikaji wa sheria za AZAKI lilotengenezwa na Mtandao. Pamoja na hayo, Mratibu awashauri Haki Zetu kuendelea kufanya kazi na kuainisha na mpango kazi wa serikali wa miaka mitano, ili kuonesha mchango wao katika jamii. Lakini pia ameiahauri taasisi ya Haki Zetu Kuwa naa Sera ya Usalama, kufanya Kazi kwa mashirikiano na taasisi wanachama wa Mtandao na kushiriki katika vikao vya Kanda na kuipongeza taasisi kwa kazi nzuri inayofanya katika Jamii inayowazunguka.

Imetolewa na;
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Agosti 10, 2021