Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC ametembelea taasisi ya EMEDO inayojihusisha na mazingira Pamoja na utunzaji wa rasilimali Hasa katika vyanzo vya maji na shughuli za Uvuvi, lakini pia kuijengea uwezo jamii hasa wanawake wanaojishughulisha na shughuli za Uvuvi katika utunzaji wa rasilimali za asili Pamoja na kujengewa uwezo na kuielimiaha jamii nafasi ya mwnaamke katika sekta ya Uvuvi ambayo imekuwa ikiwatambua wanaume pekee.

Tumekuwa tukihamasisha uhusishwaji wa wanawake katika sekta ya Uvuvi ambayo imeweza kutoa Ajira kwa asilimia 90% huku kundi la wanawake likichukua asilimia 40% pekee tena katika biashara ndogondogo ikiwemo uchuuzi, ukaangaji wa Pamoja na usafishaji wa samaki au dagaa.

Taasisi ya EMEDO imekuwa ikishirikiana na Wizara na kufanikiwa kianzisha vikundi Vya wanawake wanaofanya Kazi katika sekta ya Uvuvi, lakini pia taasisi ya EMEDO ni Miongoni mwa mashirika waanzilishi wa FISHNET ambalo Lina washirika kutoka Nchi 30 duniani.

EMEDO imekuwa ikifanya Kazi na klabu za mazingira vyuoni ambapo imefanikiwa kuanzisha klabu ya Mazingira katika chuo Cha SAUT, na hiyo ni katika kuwahamasisha vijana katika utunzaji wa mazingira lakini pia klabu hizi zimewasaidia watoto wa kike kutambua Haki zao na kuwaongezea kujiamini.

Taasisi ya EMEDO Bado inakumbana na changamoto ya upatikanaji wa Ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini, uelewa mdogo wa Haki za wavuvi, kutokuwepo kw takwimu sahihi za wavuvi wanaokimbwa na madhila pindi wawapo katika shughuli za Uvuvi, ukosefu wa vibali wakati taasisi zinataka kufanya tafiti mbali mbali katika sekta ya Uvuvi.

Taasisi ya EMEDO Bado haijawa Mwanachama wa Mtandao wa THRDC na ipo katika harakati za kujiunga na Taasisi Ili kwa Pamoja taasisi iweze kuungana na Watetezi wengine wa Haki za Binadamu katika shughuli za utetezi.

Mratibu ameishauri taasisi ya EMEDO kushirikiana na taasisi nyingine Nchini Ili kufikia maendeleo ya kitaifa lakini pia ameipongeza taasisi ya EMEDO kwa kufanya Kazi kwenye eneo ambalo ni mashirika machache yamekuwa yakijikita kufanyia kazi, lakini pia ameihamasisha taasisi kufanya utaratibu wa kujiunga na Mtandao Ili kuweza kushirikiana kwa ukaribu zaidi.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Agosti 10, 2021