Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa akiongozana na Afisa dawati la wanachama Bi Lisa Kagaruki, Pamoja Mratibu wa Kanda ya Ziwa, Bi Sophia Donald wametembelea shirika la NUMET.

NUMET ni chama cha kiuanachama kinachotetea haki za wafanyakazi kwenye sekta ya nishati na madini Tanzania. Kati ya mambo mengi, NUMET ina ofisi katika ngazi tatu; Ngazi ya matawi, ngazi ya kanda, na ngazi ya taifa. Kila ngazi ina uongozi wake ambao majukumu yake yapo kikatiba, na ni wa miaka mitatu tu.

Kazi kubwa zinazofanywa na Chama Cha NUMET ni kudai, kulinda, kutetea haki na kuboresha matakwa ya wafanyakazi hao. Hadi sasa, NUMET ina takribani wanachama 4,000 kati ya wanachama 15,000 walio katika ajira rasmi kwenye sekta ya nishati na madini. Pia NUMET ina matawi hai 32, na matawi yasiyofanya kazi 10.

Chama Cha NUMET kinakiri kukabiliana ma Changamoto zinazowakabili kadha wa kadha kama 1) Changamoto za kisheria hasa Sheria zinaruhusu madai ya ongezeko la mishahara, lakini hazijaweka taratibu rafiki za namna kukamilisha taratibu hizo za madai, Changamoto kwa upande wa mamlaka za sheria, kama Mahakama ambapo Kumekuwa na upungufu mkubwa wa majaji wanaoskiliza kesi hizi, ambapo kuna takribani uskilizwaji wa kesi 360 kwa jaji mmoja wa Mahakama kuu, Changamoto za kiusalama kwa kupokea vitisho kutoka kwa waajiri wa wafanyakazi wanaolalamikia baadhi ya makampuni yenye nguvu, Changamoto ya Rasilimali fedha ambazo huhitajika katika uendeshaji wa mashauri mahakamani.

NUMET imepata mafanikio mengi ikiwemo Kusimamia kesi kadhaa zenye mafanikio kamaa kesi ya Consolidated Labour Revisions No. 16 and 17 of 2018, ISAAC SULTAN V NORTH MARA GOLD MINES LIMITED iliamriwa tarehe 26.07.2019 na jaji Galeba ambayo mahakama iliamuru walalamikaji kupatiwa malipo ya Miezi 80 ikiwa ni Jumla yaa Shilingi bilioni 5 za kitanzania, kwa upande wa wafanyakazi pia Wameweza kuwajengea uwezo wafanyakazi juu ya umuhimu wa kuwa sehemu ya chama cha NUMET, Kufanikiwa kuwapatia Haki wafanyakazi waliovunjiwa haki zao za msingi kama waajiriwa, NUMET imeweza kuunda mahusiano mazuri na wadau mbalimbali kama vile AZAKi.

NUMET imekiri kuwa tayari kushirikiana na Mtandao na mashirika mengine katika fursa mbalimbali za kujengea watu uwezo juu ya haki za wafanyakazi

Mratibu THRDC alipata wasaha wa kuelezea juu ya jarida la uwajibikaji wa sheria za AZAKI lilotengenezwa na Mtandao. Pamoja na hayo, Mratibu ameonyesha nia ya kushirikiana na NUMET katika kutengeneza kitini/kijarida linaloelezea juu ya haki za wafanyakazi na kuishauri NUMET kuendelea kufanya kazi na kuainisha maeneo yanayohusu Kazi zinazofanywa na Chama iwapo yametajwa katika mpango kazi wa serikali wa miaka mitano, ili kuonesha mchango wao katika jamii.

Imetolewa na;
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Agosti 10, 2021