ZIARA YA MRATIBU KITAIFA WA THRDC PAMOJA NA AFISA DAWATI LA WANACHAMA YA KUWATEMBELEA WANACHAMA WA THRDC MKOANI ARUSHA

Leo tarehe 13/02/2020, Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Bw. Onesmo Olengurumwa akiongozana na Afisa Dawati la Wanachama – THRDC Wakili Joyce Eliezer walianza ziara ya kuwatembelea wanachama wetu walioko Arusha. Mashirika yaliyotembelewa leo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzani (TAWLA) mkoani Arusha.

[envira-gallery id=”5853″]

Baada ya kuyatembelea mashirika hayo Mratibu Bw. Onesmo Olengurumwa amefurahishwa na kazi mbalimbali wanazozifanya wanachama wetu katika kutetea haki za binadamu.