Mratibu Kitaifa wa Mtanda wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Bw. Onesmo Olengurumwa, akiambatana na mratibu kanda ya pwani ya kusini, Bw. Clemence Mwombeki pamoja na afisa dawati la wanachama, Bi. Lisa Kagaruki hii leo wametembelea shirika la The Path to Comfort for Women and Youth Tanzania (PWY) lililopo mkoani Mtwara.

Shirika hili lilianzishwa mwaka 2019 na limejikita kwenye kupambania haki za binadamu kupitia mlengwa wa kuwawezesha kiuchumi kwa njia mbali mbali kama kuelimishana, na kupeana fursa.

Miezi 3 baada ya kuanzishwa, tulifanya mafunzo kwa wamama 60 kuwajengea uwezo kiuchumi. Mradi wetu wa kwanza tulipokea kutoka SwissAid, mradi uliohusu masuala ya UVIKO19. Kutokana na uchanga wetu, DHWYT ndio walikua wasimamizi wetu kifedha juu ya mradi huo. Baada ya hapo fursa zikawa endelevu.

PWY inashirikiana pia na wadau mbalimbali kama vile We-World, DHWYT, Sauti ya Vijana, TWCC, T-LED, NERIO, CHPO,VSO.

Shirika hili liliona umuhimu wa kujinetwork na mitandao mbalimbali kama fursa ya ukuaji. Wao ni sehemu ya MTWANGONET, THRDC na TENMET wametuma maombi.

Kati ya mafanikio mengi, PWY imewafikia watu zaidi ya 3,000 kwenye shughuli zao.

Pamoja na hayo, PWY inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo:
• Ukosekanaji wa wafanyakazi endelevu ili kustawisha ukuaji wa taasisi.

Bw. Onesmo amewapongeza PWY kwa kazi kubwa ndani ya muda mfupi waliofanya kazi. THRDC imejiskia faraja kuwa kama wadhamini kwenye miradi ya COVID kupitia SwissAid na ndio ulikua mradi wa kwanza kwa PWY. Huu umethibitishwa kuwa ni umuhimu wa kuwa sehemu ya mtandao. Mratibu Kitaifa awashauri kuendeea kufanya kazi kwa bidii na kujitahidi kufanya ukaguzi na kutimiza majukumu ya kisheria ili wafadhili waendelee kuwaamini.

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Oktoba 18, 2021