Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, Bw. Onesmo Olengurumwa, akiambatana na Mratibu wa Kanda ya Pwani ya Kusini Bw. Clemence Mwombeki, pamoja na Afisa Dawati la Wanachama, Bi. Lisa Kagaruki hii leo wametembelea Mtandao wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Mtwara (MTWANGONET) lililopo katika manispaa ya Mtwara.

MTWANGONET ni mtandao unaofanya kazi ya kuunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali kwa wilaya ya Mtwara, kwa kuwaongezea umoja wao, kuyatafutia fursa, kuwezesha mashirika wanachama kupashana habari za fursa pamoja na kufanya utetezi wa haki za binadamu, na kuzijengea uwezo asasi za kiraia wanachama wa Mtandao.

MTWANGONET ni taasisi inayowakilisha Asasi za Kiraia katika halmashauri tatu, huku ukiwa na wanachama 42 katika ngazi ya wilaya. MTWANGONET pia ni wanachama wa mitandao mbalimbali ikiwemo THRDC na MRINGO.

Akizungumza na Waratibu THRDC waliotembelea Mtandao, Katibu wa Taasisi ya MTWANGONET, Bw. Deogratius Makoti imeushukuru Mtandao kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia wanachama wake kuweza kushiriki katika mkutano mkuu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali na Rais uliofanyika jijini Dodoma mnamo Oktoba 2021, pamoja na usaidizi wa kuwezeshwa katika kuandaa mpango mkakati wa shirika ambao umeliwezesha shirika kupata ruzuku kwa ajili ya kujiendesha kwa mwaka 2020.

“Tumekuwa wanachama wa mitandao mingi, lakini tunaushukuru mtandao wa THRDC kwa kuwa mtandao pekee unaofanya kazi kubwa katika kutulea vizuri na kutuwezesha kufanya kazi zetu kwa ufanisi zaidi, hasa katika uandaaji wa mpango mkakati (Strategic Plan 2020/2024) ambao umewafanya wafadhili kutuamini zaidi na kutupatia nafasi ya kushiriki kwenye miradi mbalimbali” Deogratius Makoti

MTWANGONET bado unakumbana na changamoto kadhaa;
• Ukosefu wa rasilimali fedha,
• Taasisi kutokuwa na uwezo mkubwa wa kuandika miradi ambayo mara nyingi imekuwa ikipatikana kwa ufinyu sana.

Bw. Onesmo Olengurumwa aupongeza mtandao wa MTWANGONET kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujitolea kuwaleta pamoja mashirika mengine wilayani humo. Awashauri pia kutumia njia mbalimbali za kuendesha shirika hili la uanachama, ikiwemo ada za wanachama. Pia MTWANGONET washauriwa kuwa karibu na wanachama wao na kufanya shughuli jumuishi zitakazowajumuisha wanachama wote wa Mtandao huo.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
 Oktoba 17,2021