Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa Akiwa na Afisa Dawati la Wanachama THRDC Bi Lisa Kagaruki wametembelea taasisi ya Tanzania Mission to the Poor and Disabled (PADI) iliyopo Manispaa ya Songea.

Taasisi ya PADI imeanzishwa mwaka 1999, likiwa linafanya Kazi katika maeneo ya Utoaji wa msaada wa kisheria, utoaji wa huduma kwa wazee Pamoja na kuwaundia mabarazavali mbali, taasisi Ina watumushi 45 wenye mikataba ambao wamekuwa wakiisaidia taasisi kutimiza wajibu wake kwa jamii.

Taasisi imefanikiwa kununua ardhi ya kutosha katika Mkoa wa Ruvuma na njombe ambayo inaweza kulisaidia Shirika kujiendesha pale wanapokosekana wafadhili.

PADI imefanikiwa kufanya mradi wa ‘Watching Boys to men’ mashuleni ambao hutumia mbinu mbali mbali kuwafunza vijana wa kiume maadili na kuwafanya Kuwa wanaume bora na kupunguza utoro mashuleni.

Taasisi imefanikiwa kuendesha mradi ambao umesaidia kuwapeleka VETA vijana 305 walioshindwa kuendelea na shule, kwa kozi fupi na kupatiwa mitaji ya kununulia vifaa vya kufanyia kazi.

Pamoja na Kazi kubwa inayofanywa PADI katika kuisaidia jamii ya mkoa wa Ruvuma, bado inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo.

• Kutokuwa na miradi endelevu inayoweza kulisaidia Shirika kufanya shughuli kwa Muda mrefu.
• Kutokuwa na fedha za kutosha kulipa wafanyakazi wa kutosha katika taasisi na kusababisha wengi kukimbia taasisi.

• Ugumu katika upatikanaji wa ‘charitable Status’ ambao ungeiwezesha taasisi kupata msamaha wa kodi mbali mbali na kuweza kuweza kujiendesha.

Naye Mratibu THRDC, Bw. Onesmo Olengurumwa ameipongeza taasisi ya PADI kwa kufanya kazi nzuri na kuikaribisha kujiunga kuwa mwanachama wa Mtandao Ili kuweza kupata nafasi ya kufahamiana ma Watetezi wengine wa Haki za Binadamu na kujua fursa mbali mbali zinazopatikana katika sekta.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
20 Oktoba, 20211 Comment

Comments are closed.