Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa hii leo ametembelea shirika la Lindi Women Paralegal Aid Centre (LIWOPAC)

LIWOPAC ni Shirika linalojihusisha na utoaji wa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto, kuwasaidia kujua Haki zao na kuzisimamia. LIWOPAC imeanzishwa mwaka 2001 na imekuwa likishirikiana na jamii Ili kuongeza uelewa juu ya haki mbalimbali katika maswala ya utokomezaji wa ndoa na mimba za utotoni.

“Kina mama wengi hawafahamu haki zao kutokana na mila na desturi kandamizi zinazowazunguka, lakini watoto ni waathirikika wakubwa zaidi wa matukio haya ya ukatili” lakini tunachojivunia ni kwamba tangu tumeanzisha shirika hili mwaka 2001 tumeweza kuisaidia jamii kwa kiasi kikubwa jamii yenyewe inakiri kusaidika Kazi na miradi yetu” Cosma Bulu Mkurugenzi LIWOPAC kuhakikisha

LIWOPAC inaeleza kuwa, kutokana na kuona uhitaji wa msaada wa kisheria katika mkoa wa Lindi ni mkubwa, shirika linaonelea ni vyema kuanzisha Paralegal Units ambazo zipo 6 kila wilaya zinazoweza kuisaidia jamii kupata haki zao katika maeneo yao hii imepelekea kuwa na wasaidizi wa kisheria zaidi ya 100 mpaka sasa.

“Tuna paralegal units 6 kila wilaya ambazo zinatoa msaada wa kisheria, wamejengewa uwezo na wanatoa msaada chini ya ufadhili wa LSF” Cosma Bulu, Mkurugenzi LIWOPAC

Katika Utoaji wa msaada wa kisheria Mkurugenzi wa LIWOPAC anaeleza kwa undani aina ya kesi zinazopokelewa na kufanyiwa Kazi zaidi na Shirika kama ifuatavyo,

“Kesi zinazopokelewa na kufanyiwa Kazi zaidi na Shirika ni kesi za matunzo ya watoto, kesi za ndoa na Talaka Kutokana na mfumo wa ndoa za mitara ulioenea zaidi mkoani Lindi” Cosma Bulu Mkurugenzi LIWOPAC

Pamoja na mafanikio haya LIWOPAC inakumbana na changamoto za kifedha ambazo zinachangia kushindwa kufanikisha baadhi ya Kazi ikiwemo kuajiri mawakili wanaoweza kusimamia mahaauri mahakamani na hivyo kuwatumia wasaidizi wa kisheria pekee, mfumo dume wa jamii ambao hupelekea ushiriki mdogo wa wanawake katika Utoaji wa Taarifa pindi wanapokumbana na changamoto za ukatili wa kijinsia, Changamoto za kutokuwa na uelewa wa mfunzo ya kiusalama na kupelekea taasisi kutoa Taarifa za Taasisi kwa watu wa Nje ya Ofisi jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa taasisi. Hata hivyo Mratibu THRDC ameishauri taasisi ya LIWOPAC kuhakikisha inakuwa na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu Ili kuweza kuonyesha Kazi zinazofanywa na Shirika katika utetezi wa Haki za Binadamu.

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
16 Oktoba, 2021