Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Bw. Onesmo Olengurumwa Akiwa na Afisa Dawati la Wanachama THRDC Bi. Lisa Kagaruki hii Leo wametembelea taasisi ya The African Institute for Comparative and International Law (AICIL).

AICIL ni shirika lililoanzishwa mwaka 2007 kama kituo, chenye lengo la kutoa huduma ya msaada wa kisheria, kufanya tafiti na kuchapisha majarida.

Mwaka 2011 kituo kilisimamisha uchapishaji wa majarida na kuendelea na Utoaji wa msaada wa kisheria.

Mwakaa 2019 kituo kikabadilishwa kuwa NGO na kuendelea na utoaji wa msaada na elimu ya kisheria kwa makundi na vijiji mbalimbali Manispaa ya Songea, pamoja na utoaji wa elimu ya afya.

Shirika limefanikiwa kuwa na mtambo utakaowezesha shirika kutoa mafunzo ya kisheria kwa jamii kwa jamii kwa kutumia (toll number) ambayo jamii inaweza kupiga namba ambayo itakuwa inatoa elimu moja kwa moja kupitia simu popote mtu alipo bila kufika ofisini.

Taasisi imefanikiwa…
1) kujitangaza na kujulikana na jamii kwa kiasi kikubwa kwa kutumia redio kwa vipindi vya elimu ya kisheria.

2) Kushirikiana na mashirika mbali mbali, Wadau, viongozi wa kisiasa, katika maeneo ya majeshi ambapo Shirika limewahi kupokea maombi ya kutoa Mafunzo ya sheria katika jeshi.

3) Shirika alimefanikiwa kujifunza na kuweza kutoa elimu ya ujasiriamali wa utengenezaji wa sabuni kwa jamii.

4) Kutoa elimu ya afya kwa jamii, pamoja na usaidizi wa utoaji wa taulo za kike wa wanafunzi wa vijijini.

5) Kusaidia katika kutatua tatizo la maji katika shule na kuwawezesha watoto wa kike Kuwa na uwezo wa kuhudhuria shule wakati wote hata katika siku za hedhi.

6) Shirika limeweza kujiingiza katika maswala ya ujasiriamali kwa kuanzisha ufugaji wa samaki na kufanikiwa kupata faida katika mavuno ya mwanzo.

7) Taasisi inashirikiana na wafadhili mbalimbali kuhamasisha michezo mashuleni pamoja na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wanazofanya vizuri ili kuchochea ari ya kusoma na kufaulu vizuri, lakini pia taasisi imekuwa ikiwatafutia ufadhili wanafunzi wasio na uwezo ambao wana matokeo mazuri darasani Ili kukuza elimu katika Manispaa ya Songea.

Pamoja na mafanikio na kazi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa, Taasisi inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo..

1) Kutokuwa na ruzuku za uhakika ambazo zingeiwezesha taasisi kukidhi malipo ya wafanyakazi wote wa Taasisi na hivyo kupelekea baadhi kukimbia ofisi.

2) Shirika linakumbana na changamoto ya usafiri wa uhakika katika kufikia maeneo yaliyo mbali na hivyo kusabisha baadhi ya shughuli kuchelewa hasa kipindi cha mvua.

3) Wanasheria kupatiwa maelezo yasiyo sahihi Kutoka kwa wateja na kupelekea mawakili kupata wakati mgumu baada ya kuendesha mashauri na kuonekana kukosa taarifa muhimu katika kesi.

Kukosekana kwa taarifa za mrejesho kutoka kwa wateja baada ya kuunganishwa na mawakili na hivyo kuizuia taasisi kupata taarifa za maendeleo ya kesi kwa ajili ya rekodi za shirika.

Katika kutatua changamoto ya kifedha, taasisi imeanza mradi wa ununuzi wa mahindi na kuuza serikalini ili kuliwezesha shirika kujiongoza zaidi pindi kunapokosekana ruzuku kutoka kwa Wafadhili.

Mkurugenzi anaeleza namna THRDC imeshiriki katika kuisaidia taasisi kufikia malengo mbali mbali…

“THRDC imetusaidia sana katika utengenezaji wa mpango mkakati ambao umesaidia marafiki wa shirika kujua dira yetu katika shughuli za utetezi na kutuamini kutupatia ruzuku. Mtandao umetusaidia kuongeza mashirikiano kwa kukutana na watetezi wengine wa haki za binadamu na kujifunza mbinu za ujasiriamali ambazo zimezaa matunda katika taasisi yetu” Agnes Haule, Mkurugenzi AICIL

Hata hivyo Mratibu THRDC ameipongeza taasisi ya AICIL kwa Manispaa ya Songea na mkoa mzima wa Ruvuma na ameishauri kuendelea kujenga mahusiano mazuri na mahakama pamoja na ustawi wa jamii Ili kuhamasisha ufuatiliaji na kuwezesha kesi kukamilika kwa wakati.

Pia Olengurumwa ameishauri taasisi kuwa na utaratibu wa kutunza kumbukumbu za miradi kwa namna taasisi imewafikia watu, lakini pia kufanya kazi kwa kuendana na taratibu na sheria mbali mbali zilizowekwa na nchi.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
19 Oktoba, 2021