Mwanza.

Mratibu Kitaifa akiongozana na Afisa wa Mtandao, watembelea shirika la Mikono Yetu Centre For Creativity and Innovation (Mikono Yetu).
Mikono Yetu ni shirika lililosajiliwa kisheria na linaendesha programu nne mpaka sasa. Programu zote zimejikita katika masuala ya haki ya mwanamke na msichana. Programu hizi ni;
1) Uwezeshaji wanawake kiuchumi (Women Economic Empowerment)
– Programu hii inahusisha ujasiriamali kwa upande wa mwanamke, na kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa viwanda vya usindikaji kwa ajili ya kuongeza thamani ya bidhaa zao. Programu hii ina jumla ya vikundi 6 vya wanawake katika eneo la Sengerema.

2) Uwezeshaji Wasichana (Girls Empowerment)
– Programu hii inafanya kazi kwa bango kubwa la “Msichana ni Tai” iliyoanza mwaka 2019 kwa udhamini wa NOVA Foundation. Programu hii inahusika na kuwajengea uwezo wasichana wenye umri wa miaka 9-20, walioko nje ya shule. Kwa sasa imewafikia wasichana 445 kwa kata ya Buswelu. Kupitia hii programu, msichana hujiona wa thamani katika jamii kwa kuweza kufikia ndoto zao. Kwa mfano, uanzishaji wa “Msichana TV” ambayo ni TV yenye ndoto kubwa sana. Pia wasichana hawa hupewa elimu ya uzazi.

3) Programu za Mazingira kwa wanawake.
4) Ukatili wa Kijinsia (GBV) Program.

Changamoto
Mikono Yetu hupata changamoto mbalimbali katika kazi zao, ikiwemo;
– Janga la UVIKO 19
– Upatikanaji wa vibali vya kufanyia kazi kutoka kwa mamlaka husika
– Changamoto kutoka kwa jamii, hasa wazazi/walezi wa wasichana
– Changamoto za kifedha katika jamii zinazohusishwa.

Mafanikio katika ukuaji wa shirika la Mikono Yetu
-Kwa sasa, shirika lina bajeti ya 130,000 USD, wafanyakazi walioajiriwa 10, wakujitolea 3 na interns 5. Haya ni mafanikio makubwa sana kwa shirika.
– Pia kupitia mafunzo mbalimbali kutoka THRDC, Shirika la Mikono Yetu limeweza kuweka camera za usalama (CCTV Cameras), na hata maendeleo ya kifedha ni kutokana na mafunzo kutoka Mtandao.

Mratibu awahimiza juu ya kuendelea kuweka rekodi nzuri ya changamoto zinazotokana na UVIKO19. Pia kuendelea kufanya kazi na kuainisha na mpango kazi wa serikali wa miaka mitano, ili kuonesha mchango wa sekta ya AZAKI katika jamii. Mikono Yetu imeshauriwa pia kutumia ipasavyo televisheni ya Watetezi TV katika kuhabarisha jamii juu ya kazi zao, na hata kuungana na Msichana TV ili kuhabarisha zaidi.

Kuhusu Msichana TV
Ni channeli iliyoanzishwa na Mikono Yetu kupitia wasichana wenye kipaji cha uandishi wa habari. Hadi sasa, TV hii inatumia cable na inawafikia hadi watu 50,000. Wasichana hao wana maono mbalimbali ikiwemo kuendelezwa kitaaluma katika tasnia ya habari. Mikono Yetu imeweza kufanya mawasiliano ya awali na SIDO, ITV, HakiElimu na Action Aid juu ya maendeleo ya Msichana TV.

Imetolewa na;
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Agosti 9, 2021.