Baada ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria Nchini uliofanyika tarehe 23 Januari,2022, Leo tarehe 25 Jan,2022 Mkurugenzi wa shirika mwanachama wa Mtandao la Utoaji wa msaada wa kisheria Tunduru (TUPACE) Bw. John Nginga ameungana na timu ya Wilaya katika utoaji wa elimu ya sheria. Timu ya wilaya ilihusisha Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mh. Chuvaka, Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mlingoti, PP Steven wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru

Utoaji wa Elimu hiyo uliongozana na kutembelea kwa gereza kuu la Tunduru. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mh. Chuvaka alikabidhi vitu kadhaa ikiwemo sabuni, mafuta ya kupakaa n.k kwa Mkuu wa Gereza Kuu – Tunduru, kwa niaba ya timu yote iliyotembelea gerezani hapo.

Ugeni huo gerezani hapo ulilenga kuwafariji Wafungwa wa Gereza Hilo (Wafungwa Wanaume na Wanawake), sambamba na kuwaelimisha juu ya masuala ya kisheria.

Elimu ya Sheria iliyotolewa ilipokelewa na maswali mbalimbali yahusuyo Uendeshaji wa makosa Katika Mahakama ikiwemo; Kwanini Polisi anayekamata,ndiye anayepeleleza na ndiye huyo huyo anaendesha shitaka Mahakamani.
Wafungwa hao wameomba kuanzishiwa Maktaba(Library) ya vitabu vya sheria ili kujielimisha zaidi masuala ya SHERIA,

TUPACE Kupitia mkurugenzi wake, imeahidi kusaidia upatikanaji wa vitabu vya sheria vilivyoandikwa kwa lugha rahisi.
Timu hii itaendelea kutoa elimu ya kisheria hadi tarehe 29 Januari 2022 ambapo ndio kilele cha wiki hii ya sheria.

Pamoja na hayo, TUPACE itatarajia kutoa elimu ya kisheria kwa shule takribani 15 za msingi na sekondari.