Katika siku ya maadhimisho ya kutokomeza ukeketaji duniani (6 Februari), Serikali imeungana na wadau mbalimbali ikiwemo Asasi za Kiraia na wanachama wa Mtandao kupinga ukiukwaji huo wa haki za binadamu. Maadhimisho kitaifa ya mwaka huu yamefanyika wilayani Tarime mkoani Mara. Mada mbalimbali zilitolewa wakati wa maadhimisho hayo ikiwemo, “wekeza kwenye maendeleo ya bàadae ya mtoto na wawe salama dhidi ya vitendo vya ukeketaji na Dr Jane Sempeho”
Kongamano hili ni kuweka mikakati hai ya namna ya kuondoa ukeketaji kwenye jamii zetu .

Katika maadhimisho hayo, wanachama wa Mtandao mbalimbali wanaotetea haki za watoto walihudhuria ikiwemo LHRC, ESTL, C-Sema, Tuwakomboe Paralegal Organization, na Hope for Girls and Women.

Hali ya watu duniani kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya Duniani (WHO), wasichana million 200 wamekeketwa . Na kwa Tanzania, zaidi ya mikoa 10 yanafanya ukeketaji.

#Miaka10YaTHRDC
#10YrsOfTHRDC