Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yamefanyika jana tarehe 23 Januari 2022 Katika Mahakama ya Wilaya ya Tunduru. Mgeni Rasmi alikua ni Kaimu DAS, Bw. Maneno Agustino. Uzinduzi wa maadhimisho hayo kwa wilaya yameandaliwa na Mahakama ya wilaya, ambapo shirika mwanachama wa Mtandao, Tunduru Paralegal Centre (TUPACE) lilialikwa kama mmoja wa wadau wa sheria katika eneo hilo.

Wengine walioshiriki usinduzi huo ni pamoja na Hakimu Mkaz Mfawidhi, Mkuu wa Magereza, Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduru, Watumishi wa Mahakama zote Tunduru, Mawakili wa Kujitegemea pamoja Wasaidizi wa Kisheria (TUPACE).

Sambamba na Maadhimisho hayo pia imeandaliwa Ratiba ya Utoaji wa Elimu ya Sheria baadhi ya Taasisi zikiwemo Shule za Sekondari, Magereza nk Hadi Kilele tarehe 2 Februari 2022.