UWASILISHAJI WA POSITION PAPER NA ACTION PLAN YA AZAKi DHIDI YA COVID-19 WIZARANI
Wapendwa Wakurugenzi na Wadau wa Haki za Binadamu nchini,
Leo, Jumamosi ya tarehe 25 Aprili 2020, Jukwaa la Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia (AZAKI) Tanzania (CSOs Directors’ Forum) lilifanikiwa kuiwasilishia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (MOHCDGEC) position paper yetu na Action Plan ya mwaka (Mei 2020 – Aprili 2021) inayohusiana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona.Uwasilishaji huu ulifanywa na wawakilishi; Bw. Onesmo Olengurumwa (THRDC), Bi. Jane Magigita (Equality For Growth) na Bi. Ummy Nderiananga (SHIVYAWATA).
Tunamshukuru sana Mh. Waziri kwa kutupokea vizuri na baadae kutukabidhi kwa Naibu Waziri kwa ajili ya kufanya uwasilishaji huo uliodumu kwa takribani lisaa limoja. Dkt. Ndugulile alituonesha ushirikiano mkubwa sana kwa niaba ya wizara nzima, na kutupongeza sana kwa hatua hii tuliyoichukua kuja na mpango wa pamoja.
Aliongezea kuwa, hatua hii itasaidia kupima mchango wa AZAKi katika vita ya COVID-19, ukizingatia pia wao (MOHCDGEC) ndio walezi wa asasi hapa nchini.
Katika kikao hicho kifupi, tuliweza kuielezea Wizara nia yetu ya dhati kabisa ya kuunga mkono juhudi hizi kuhusu COVID-19. Vivyo hivyo, Dkt. Ndugulile ametuahidi kutenga muda na kulipitia chapisho letu, ili kuweza kujua maeneo ambayo yanahitaji ushirikiano wa moja kwa moja na Wizara katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya COVID-19.
Onesmo Olengurumwa,
Secretary – Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI Tanzania
25 Aprili, 2020