UKOSEFU WA AJENDA MAHSUSI NI CHANGAMOTO KATIKA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

Kukosekana kwa Ajenda mahsusi imeelezwa kuwa moja ya kikwazo katika kutekeleza ajenda ya Utetezi wa Haki za Binadamu nchini. Haya yameelezwa na Mkurugenzi wa PINGOs Forum Wakili Edward Porokwa wakati wa kikao cha pamoja na Mratibu Kitaifa wa THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa ambaye aliongozana na Mratibu wa THRDC wa Kanda ya Kaskazini pamoja na Wakili Joyce Eliezer ambaye ni Afisa wa Dawati la Wanachama – THRDC.

“Watetezi wengi wamejikita katika ajenda za waathirika na sio ajenda za mageuzi (transformation agenda)”, alisema Wakili Porokwa.

Pamoja na ukosefu wa ajenda mahsusi, pia Wakili Porokwa ameeleza kuwa, changamoto ya wananchi wengi ni kwamba, wengi wao hushirikiana na watu ambao ndio wanaohusika kudhulumu haki zao.