TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA (CHRAGG) KUDUMISHA UHUSIANO NA THRDC

Asubuhi ya leo maafisa kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG); Bi. Beatrice Beda (kushoto) pamoja na Bw. Mbaraka Kambona (kulia), wametembelea ofisi za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na kufanya mazungumzo na Afisa Uwezeshaji wa THRDC Wakili Deo Bwire (katikati) juu ya jinsi gani CHRAGG na THRDC wanaweza kuboresha ushirikiano katika kufanya kazi za Utetezi wa Haki za Binadamu nchini kwa ukaribu zaidi katika siku za usoni.

Huu ni mwendelezo mzuri wa mahusiano ya muda mrefu kati ya CHRAGG na THRDC, lakini pia ni mwanzo mzuri kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ikizingatiwa kuwa, ni siku 2 baada ya Rais Magufuli kuwateua rasmi Mwenyekiti mpya wa CHRAGG Jaji mstaafu Mathew Pauwa Mhina na Makamu wake Bw. Mohamed Khamis Hamad pamoja na makamishna wa Tume hiyo.

[envira-gallery id=”5686″]

Baada ya mkutano huo mfupi, wageni wetu pia waliitembelea Maktaba yetu ya machapisho yetu (Human Rights Resources Centre) na kukabidhiwa nakala za Ripoti yetu ya mwaka 2018 pamoja na Mwongozo wa Ulinzi kwa Watetezi wa Haki za Binadamu.

Imetolewa leo tarehe:
24/09/2019

Na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)