Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wameendesha mafunzo ya siku moja kwa mawakili wa TLS Kanda ya Ubungo kuhusu namna ya kuendesha mashauri yenye maslahi ya umma (Public Interest Litigation).

Mafunzo hayo yalifanyika katika Jengo la Wakili House jijini Dar es salaam na yanalenga kuwaongezea uwezo mawakili hao kuhusu dhana ya mashauri yenye maslahi ya umma na namna wanavyoweza kuendesha mashauri hayo katika mahakama za ndani na za kimataifa.

Miongoni mwa wawezeshaji katika mafunzo hayo ni Wakili Onesmo Olengurumwa,Mratibu THRDC,Wakili Nuru Maro,Afisa Uchechemuzi kutoka THRDC na Jaji Mstaafu Robert Makaramba.

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
18/09/2021