THRDC YAWAJENGEA UWEZO WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUHUSU UANDISHI WA RIPOTI ZA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU

THRDC YAWAJENGEA UWEZO WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUHUSU UANDISHI WA RIPOTI ZA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU

Dar es Salaam, Tanzania

Asubuhi ya leo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaendesha mafunzo ya siku mbili ya ufuatiliaji, utunzaji wa kumbukumbu na uandishi wa ripoti za masuala ya haki za binadamu. Mafunzo hayo yamewakutanisha watetezi mbalimbali wa haki za binadamu nchini pamoja na waandishi wa habari kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uandishi wa ripoti za masuala ya haki za binadamu.

Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya APC iliyopo Bunju jijini Dar es salaam kuanzia hii leo Agosti 5 hadi hapo kesho Agosti 6 yatakapohitimishwa rasmi. Pichani ni Wakili Leopold Mosha ambaye ni Afisa Mjenga uwezo THRDC akiwapitisha washiriki juu ya sheria zinazowaongoza watetezi wa haki za binadamu katika utendaji wa majukumu yao.

Imetolewa na:

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)