THRDC YATOA TAMKO KUELEKEA MAADHIMISHO YA 7 YA SIKU YA WATETEZI NCHINI

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) leo umetoa tamko kuelekea maadhimisho yake ya 7 ya Siku ya “Watetezi wa Haki za Binadamu” maarufu kama Defenders Day. THRDC imepanga kufanya maadhimisho hayo mnamo tarehe 2 Julai 2021, wiki chache tu kutoka sasa, katika ukumbi wa Mlimani City Julai.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umekuwa ukiadhimisha siku hii ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ama “Defenders Day” tangu mwaka 2013 kila tarehe 28 mwezi Aprili. Lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa wetu, tuliahirisha maadhimisho hayo hapo awali tarehe 28 Aprili mwaka huu.

Pia kupitia maadhimisho haya, THRDC kwa miaka mingi sasa imekuwa ikishirikiana na wanachama wake, wadau wa maendeleo, Watetezi wa Haki za Binadamu, na hususani Mamlaka za kiserikali, kwa nia ya kuimarisha mahusiano kati ya Watetezi wa Haki za Binadamu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Maadhimisho ya Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu yamekuwa yakihudhuriwa na Wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali. Mwaka 2017 mgeni rasmu katika Maadhimisho ya 4 ya Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ambaye sasa ni Rais) Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliwakilishwa na Mh. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) Waziri wa Katiba na Sheria. Mnamo mwaka 2018, mgeni rasmi katika maadhimisho ya 5 ya Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania alikuwa ni Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleimani Jaffo ambaye aliwakilishwa na Mhe. Joseph Kakunda (MB) aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Na mwaka 2019, mgeni rasmi katika maadhimisho ya 6 ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania alikuwa Mhe. Isaac Kamwelwe aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi ambaye aliwakilishwa na Mlembwa Mnaku aliyekuwa kiongozi wa Idara ya TEHAMA katika Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Mwaka 2020 hatukufanya maadhmisho kutokana na changamoto za Korona.

Mwaka huu, THRDC inatarajia kuwaleta pamoja Watetezi wa Haki za Binadamu wapatao 300, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Viongozi wa Kiserikali na Mahakama, Wadau wa Maendeleo, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Vyombo vya Habari pamoja na wadau mbali mbali wa haki za Binadamu ambao wote watakutana katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ili kujadili maswala mbalimbali kuhusiana na Mchango wa Asasi za Kiraia katika Maendeleo ya Taifa.

Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Kujadili mchango wa Asasi za Kiraia katika Utekelezaji wa Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Taufa wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/26)” ambapo asasi za kiraia zikiwa kama moja ya sekta muhimu katika maendeleo ya taifa, zimeonyesha nia katika kuchangia maendeleo.

Aidha, zaidi ya mashirika 300 yakiwemo mashirika wanachama wa THRDC, yameshatengeneza Mpango wa Asasi za Kiraia wa Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Taifa (2021/22 – 2025/26). Mpango huu wa utekelezaji utakabidhiwa kwa Waziri Mkuu wakati wa maadhimisho ya 7 Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, kuashiria mwendelezo wa kazi zinazofanywa na watetezi wa haki za binadamu/AZAKI katika kukuza maendeleo ya taifa.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

Leo tarehe 22 Juni 20211 Comment

  • Hello partners i like to ask you kindly to extend an invitation to us as organization to attend this very auspicious event on friday, we as human rights activists, advocacy team, also as human rights young practitioners. Our organization called Mwambao Agriculture Development Organization -MWADO – we are located at Mkuranga as our headquarter. You may reach by this email of mine as of director there.

    Regards

    Issa Isihaka 0788257640

Comments are closed.