THRDC YATEMBELEWA NA WAKUTUBI KUTOKA UDOM

Mapema leo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ulitembelewa na Wakutubi kutoka Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakiongozwa na Dr. Josephine Wilfred.

Dhumuni la ujio wao lilikuwa kukusanya machapisho na ripoti mbalimbali za Mtandao kwaajili ya matumizi ya wanachuo kwenye Maktaba ya Chuo Kikuu cha UDOM.

Pichani ni wageni hao wakipokea machapisho ya THRDC kutoka kwa James Laurent, Afisa Kavazi wa THRDC.

Imetolewa na THRDC,

Leo tarehe 24 Juni 2021