Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania ( THRDC) umesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani Euro 180,000 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 470 na Shirika la Frontline Defenders lililopo nchini Ireland ili kuimarisha utekelezaji wa Mpango mkakati wa taasisi unaolenga kulinda na kuwaongezea uwezo Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania.

Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi tarehe 05/10/2021 na utekelezaji wake utaanza mapema mwezi huu na kumalizika mwaka 2022.Fedha hizi zitatumika kuendeleza kazi za taasisi za utoaji mafunzo mbalimbali kwa watetezi wa haki za binadamu nchini, kuwatetea watetezi wa haki za binadamu hasa wanaopitia changamoto mbalimbali na kuchangia utekelezaji wa sera za taasisi kwa ujumla .

Wanufaika wa mradi huu ni watetezi wa Haki za Binadamu, pamoja na Wadau mbali mbali wa serikali huku mradi huu ukitarajiwa kuongeza nguvu Katika utetezi wa haki za binadamu nchini na kuboresha mahusiano kati ya Watetezi na taasisi mbalimbali za kiserikali.

Imetolewa na

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadaamu
Octoba 7,2021