THRDC YAPATA UGENI

Mapema leo tulitembelewa na Mkurugenzi wa shirika la Maasai Pastoralist Development Organization Ndugu Lebaraka Laizer.

Katika ugeni huo Ndugu Lebaraka Laizer aliambatana na Afisa programu Ndugu Amani Sekino pamoja na Mhasibu Ndugu Elibahati Matulo ili kujionea na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na THRDC.

Pichani ni Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) akimkabidhi Mkurugenzi wa shirika la Maasai Pastoralist Development Organization baadhi ya machapisho ya THRDC.

Imetolewa na THRDC
Leo Julai 23, 2021