Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),leo Agosti 31,2021, umetembelewa na Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Youth Behavioural Change Organization ( TAYOBECO),Bi.Shida Kabulunge.

Katika Ugeni huo Bi.Shida Kabulunge ameambatana na Afisa Tathimini na Ufuatiliaji( M& E) Ndugu Adinani Mussa pamoja na Mshauri Mwelekezi( consultance),Ndugu Rodgers Fungo ili kujionea na kujifunza kazi mbali mbali zinazofanywa na Mtandao huo ikiwa ni pamoja kujua taratibu za kujiunga kuwa mwanachama wa Mtandao

Pichani ni Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu akimkadithi Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Youth Behavioural Change Organization baadhi ya machapisho ya Mtandao.

Imetolewa na:
Dawati la Wanachama – THRDC
Agosti 31,2021