Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umeongeza mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Euro $235,975 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 600 na Shirika la Protection International Kenya (PIK) ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mradi wa miaka miwili ulioanza mwaka 2020 unaolenga kukuza mahusiano kati ya asasi za kiraia na serikali ili kuimarisha shughuli za utetezi wa haki za binadamu nchini.

Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi tarehe 29/11/2021 na Utekelezaji wake utaanza mapema mwezi December na kumalizika mwaka 2022.

Fedha hizi pia zitatumika kutoa mafunzo mbalimbali kwa watetezi wa haki za binadamu, kufanya mikutano ya kimkakati na serikali inayolenga kuboresha hali ya haki za binadamu inchini, pamoja na kuwatetea watetezi wa haki za binadamu.

Shirika la Protection International of Kenya (PIK) limekuwa likiifadhili THRDC tangu mwaka 2020 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya mtandao wakiwa ni Wadau wakubwa wa Haki za Binadamu nchini Tanzania.

Imetolewa na THRDC
03/12/2021